WAZIRI UMMY AZINDUA MAKASHA YA USAMBAZAJI KONDOMU NCHINI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu akizindua makasha ya kusambazia kondomu katika hafla iliyofanyika katika Stendi Kuu ya Mkoa wa Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania Youth Alliance, Peter Masika.

Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthonya Mavunde akijaribu kununua kondomu kwenye kasha

Makamu Mwenyekiti wa Kamati wa Kudumu ya Bunge, Christina Mzava akinunua kondomu ya sh. 1000 kupitia kwenye kasha hilo maalumu la kuuzia

Mkurugenzi Mtendaji wa Tayoa, Peter Masika amesema taasisi hiyo ambayo inahusika na kuwaendeleza vijana kiuchumi na wameaamua kuwekeza katika kuwakinga vinaja dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa vile ugonjwa huo unamaliza nguvu kazi katika Taifa

 

Baadhi ya wageni waalikwa na vijana wa Tayoa wakiwa katika hafla hiyo

Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe akizungumza wakati wa uzinduzi wa makasha hayo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt Fatma Mganga akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Kikundi cha ngoma kikiburudisha

Waziri Ummy akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru (katikati) pamoja na Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Ummy Mwalimu amezindua makasha ya kusambazia kondomu katika hafla iliyofanyika katika Stendi Kuu ya Mkoa wa Dodoma.
Amezindua kasha maalumu la kuuzia kondomu mpya aina ya safari ambapo mteja anaingiza noti ya sh. 1000 na kutoa pakiti yenye kondomu tatu  zenye viwango ambapo pia amezindua kasha lenye kondomu  za bure aina ya Zana.

Waziri Ummy ameipongeza Taasisi ya Tanzania Youth Alliance (Tayoa) kuisaidia sarikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi na kwamba licha ya hivi sasa serikali kuelekeza nguvu kwenye mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa Korona, lakini Tayoa hawajaacha ajenda yao ya kupambana na ugonjwa huo wa Ukimwi.

“Nawapongeza kwa kufocus katika suala la mapambano dhidi ya Ukimwi nchini,  hivi sasa dunia nzima inapambana na UVIKO 19, lakini wao bado wako ngangari kupambana na  virusi vya Ukimwi, nampongeza Mkurugenzi wa Tayoa Peter Masika na timu yake yote,” hongereni

“Wakati dunia inapambana na janga la corona jamii isijisahau katika kupambana na  magonjwa mengine ambayo ni hatari zaidi ukiwemo ugonjwa wa ukimwi ambapo ripoti inaonesha vijana ndio wanaathirika zaidi ambapo kati ya vijana 100 vijana 40 wameathirika,”amesisitiza Waziri Ummy.

Amesema kuwa takwimu za afya zinaonesha kwa mwaka watu elfu 72 wanapata maambukizi ambapo kwa saa moja watu 8 hupata maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.

Amewataka Tayoa kusambaza makasha hayo katika vijiji, kata kwenye Halmashauri zote 184 nchini ambapo hivi sasa wameshasambaza katika Halmashauri na lengo ni kusambaza takribani kondomu mil. 7.6.

Pia amewapongeza Tayoa kuajiri vijana 40,000 nchini watakaosimamia mauzo ya kondomu aina ya safari ambapo kila sh. 1000 muuzaji atapata asilimia 30 ambayo ni sh. 300 kwa kila pakiti.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tayoa, Peter Masika amesema taasisi hiyo ambayo inahusika na kuwaendeleza vijana kiuchumi, wameaamua kuwekeza katika kuwakinga vijana dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa vile ugonjwa huo unamaliza nguvu kazi katika Taifa.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Mganga, Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwanfupe, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabir Shekimweri, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru, Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madwa ya Kulevya, Christina Mzava na viongozi wa wizara ya Afya na Tamisemi

 

 

Leave A Comment

Categories

At vero eos et accusamus et iusto odio digni goikussimos ducimus qui to bonfo blanditiis praese. Ntium voluum deleniti atque.

Melbourne, Australia
(Sat - Thursday)
(10am - 05 pm)
Choose Demos Submit a Ticket Purchase Theme

Pre-Built Demos Collection

Consultio comes with a beautiful collection of modern, easily importable, and highly customizable demo layouts. Any of which can be installed via one click.

Cryptocurrency
Business Construction
Business Coach
Consulting
Immigration
Finance 2
Corporate 1
Corporate 2
Corporate 3
Consulting
Business 1
Business 2
Business 3
IT Solution
Tax Consulting
Human Resource
Life Coach
Marketing
Insurance
Finance RTL
Marketing
Consulting
Consulting
error: Content is protected !! Please contact to Tayoa for more help